Wapendwa Wazazi na Walezi,
Utafiti huu wa maswali 11 unatoka kwa Shirika la Elimu ya Kitaifa la Vermont. Lengo hapa ni kuwasaidia walimu pamoja na wafanyikazi wengine wa shule ili waweze kukusaidieni vyema nyinyi na watoto wenu katika kipindi hiki cha dharura ya kiafya ya janga la Covid-19. Tunafahamu ya kwamba hiki ni kipindi kigumu na kisichoeleweka kwenu - kuyashughulikia majukumu ya wazazi, kusimamia uzingatiaji wa mafunzo ya mbali au mtandaoni, na kujitafutia riziki - na hata kwa watoto wako, ambao wametengwa na marafiki wao, shule, na shughuli z ao za kawaida.
Taarifa hiyo itawasaidia walimu kuimarisha utaratibu wa mafunzo ya mbali au mtandaoni, kuweka viwango bora vya matarajio kwako na kwa watoto wako, kuitambua mikingamo ya hali ya kifamilia, na kupunguza msongo wa mawazo. Kadhalika, itatusaidia kufanya kazi na bunge, gavana na wengineo ili kukulinda pamoja na familia yako kutokana na matatizo ya kifedha, kimatibabu na hasara za kiuchumi ambazo zimewakumba watu wengi mno katika kipindi cha janga hili.
Ili kuilinda faragha ya watu, HATUULIZII majina ama hata anwani za nyumbani, bali tunaulizia tu Kaunti unayoishi.
Hamu yetu kuu ni wewe kuwa heri, vyema na salama.Tafadhali fahamu ya kwamba Walimu 13,000 wa shule za Umma za NEA wa huko Vermont, wasaidizi wa kiusimamizi, wasaidizi wa walimu, madereva wa mabasi, wafanyikazi walezi na wasimamizi watakusaidia kwa njia yoyote ile watakayoweza.
Asante sana.
Wako Mwaminifu,
Don Tinney, Rais, Vermont-NEA