FARNES ZONE COMPANY STUDENT FORM  Logo
  • Student Application Form – 3 Months Course

    Apply now to join FARNES ZONE COMPANY's intensive digital skills course. Open to students worldwide for online and hybrid learning in technology, media, business, and new opportunities.
  • MKATABA WA USHIRIKIANO WA ELIMU
    Mkataba huu unafanyika kati ya:

    COMFORTER ORPHANS FOUNDATION, taasisi inayojihusisha na malezi na elimu ya watoto,
    (hapa itaitwa Comforter Orphans Foundation)

    NA

    FARNES EDUCATION, taasisi inayotoa elimu kwa njia ya mtandao (online),
    (hapa itaitwa Farnes Education).

    Pande zote mbili zinakubaliana masharti yafuatayo:


    1. LENGO LA MKATABA
    Lengo la mkataba huu ni kushirikiana kutoa elimu ya online kwa wanafunzi wa Comforter Orphans Foundation kupitia Farnes Education.


    2. MUDA WA MKATABA
    Mkataba huu utadumu kwa muda wa miezi mitatu (03) kuanzia tarehe ya kusainiwa.


    3. MFUMO WA MASOMO
    Masomo yatafanyika online.
    Kila mwanafunzi atasoma mara moja kwa wiki.
    Kila somo litakuwa na dakika 45.

    4. ADA NA USAJILI
    Kila mwanafunzi atapewa voucher kwa ajili ya kuhudhuria darasa la online.
    Hakuna ada ya kujiandikisha kwa mwanafunzi.

    5. NIDHAMU YA MWANAFUNZI
    Mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria darasa kwa wakati.
    Mwanafunzi akichelewa bila kutoa taarifa mapema, atalipa adhabu ya USD 1.

    6. KOZI, VYETI NA MAHAFALI
    Kozi zote zitakamilika ndani ya miezi 3.
    Wahitimu wote watapewa cheti cha ndani (Internal Certificate).
    Kutakuwa na sherehe ya mahafali.
    Gharama ya kupata cheti ni Shilingi 15,000/= kwa kila mwanafunzi.

    7. WAJIBU WA FARNES EDUCATION
    Kutoa masomo ya online kwa ubora.
    Kutoa walimu wenye uwezo.
    Kutoa vyeti kwa wahitimu.

    8. WAJIBU WA COMFORTER ORPHANS FOUNDATION
    Kuchagua na kusimamia wanafunzi.
    Kuhakikisha wanafunzi wanazingatia nidhamu.
    Kushirikiana kufuatilia maendeleo ya masomo.

    9. KUVUNJA MKATABA
    Upande wowote ukitaka kuvunja mkataba kabla ya muda wake kuisha, atalipa USD 15.
    Notisi ya siku 14 itatolewa kabla ya kuvunja mkataba.

    10. USIRI NA ULINZI
    Taarifa za wanafunzi zitahifadhiwa kwa usiri.
    Hakuna upande utakaotumia jina au taarifa za mwenzake bila ruhusa.
    Maslahi ya watoto yatapewa kipaumbele.

    11. UTATUZI WA MIGOGORO
    Migogoro yoyote itatatuliwa kwa mazungumzo. Ikishindikana, itafuata sheria za Tanzania.


    12. MAKUBALIANO YA MWISHO
    Mkataba huu umeandikwa kwa makubaliano ya pande zote mbili na unasainiwa kama ifuatavyo:

    SAHILI
    Imesainiwa tarehe : 01jan2026

    Kwa niaba ya Comforter Orphans Foundation
    Jina: COMFORTER MANAGEMENT

    Cheo: MANAGER

    Kwa niaba ya Farnes Education
    Jina: FARNES MANAGEMENT

    Cheo: HR Office

  • Browse Files
    Drag and drop files here
    Choose a file
    Cancelof
  • Clear
  • Should be Empty: